Viatu virefu huongeza mvuto kwa wanawake.
JOYCE MAGOTI
KARIBU wapenzi wasomaji wa safu hii ya urembo, kama ilivyo kawaida yetu kila wiki tunakutana kwa lengo la kukumbushana na kuwekana sana katika suala zima la urembo.
Kama tujuavyo kuwa urembo umechukua nafasi kubwa katika maisha yetu kwani kila moja wetu anatamani kuwa na muonekano tofauti kulingana na wakati hususan katika mavazi na mitindi mbalimbali ya urembo.
Leo katika mada yetu tunaangali juu ya uvaaji wa viatu virefu, ama hakika viatu hivi ni miongoni mwa viatu vinavyopendwa kuvaliwa katika kipindi hiki ambapo pia ni viatu ambavyo kwa kiasi kikubwa havipotei katika fasheni mbalimbali za mavazi na urembo ambapo pia huwa katika chati wakati wote.
Mvaaji wa viatu hivi hususani warembo wote wanaopenda kuonekana nadhifu na wanaokwenda na wakati muda wote wa uvaaji wa viatu hivi huonekana warembo na wenye kuvutia ambapo pia huwafanya kubadili miondoko yao na kutembea mithiri ya warembo walio jukwaani katika mashindano ya urembo.
Mara nyingi viatu hivi huvaliwa ofisini,kanisani au katika mikutanano mbalimbali ambapo mvaaji itamlazimu kutotembea kwa miguu kwa muda mrefu ili kumsadia asiumize miguu yake.
Mbali na kuwa vinaongeza urembo, viatu hivi pia ni kinga kwa ajili ya kuhifadhi miguu yako, viatu hivi hupatikana katika mitindi tofauti tofauti abavyo pia huvaliwa kulingana na sehemu husika.
Vipo viatu vya ngozi na vinavyofunika, mara nyingine viatu hivi havina ngizo asilia bali vinakuwa kama plastiki, pia vingine huwa na uwazi mdogo kwa mbele, viatu hivi hupendeza zaidi zaidi vikivaliwa kwenye sherehe na kanisani. Unaweza kuvaa kazini kama kazi yako haikulazimu kutembea tembea maana vitachosha miguu yako na kupunguza ufanisi.
Viatu hivi pia vinapendeza ukivalia na suti ya sketi au suruali, sueruali za vitambaa na blauzi nadgifu pamoja na gauni fupi au refu ambalo unaweza kuvaa ukiwa kazini au kanisani.
Viatu hivi pia vinafaa kuvaliwa usiku katika sherehe zozote kwa kuvalia na gauni refu la jioni au fupi ambapo pia huopendeza ukivalia nguo yoyote ya jioni na hukufanya uonekane tifauti katika kutembea na muonekano wako kwa jumla.
Tukutane wiki ijayo katika mada nyingine, wasiliana nami kwa barua pepe joymagoti87@yahoo.com, au 0715933823.
Mwisho.
Wali wa Biriani na Kababu.
JOYCE MAGOTI
KARIBUNI tena wapenzi wa mapishi ambapo kila wiki tunakutana hapa kwa ajili ya kufundishana mapishi ya aina mbalimbali, kama ilivyo kawaida katika masuala ya nyumbani leo nimekuandalia pishi la wali wa biriani kwa kababu.
Kwa hakika pishi hili ni linapikwa kwa asilimia kubwa na watu mbalimbali majimbani hususani wakati wa mlo wa usiku au mchana na hiyo inategemea na matakwa ya kiongozi wa familia hiyo ambaye anapana masuala ya chakula katika familia yake.
Mahitaji ya pishi hili pia hayana yanapatikana kwa urahisi katika mazingira tunayoishi hasa katika masoko ya nafaka, na katika maduka yoyote yanayouza nafaka na halihitaji gharama kubwa kuliandaa na kupika
Vipimo vya Kababu:
Nyama ya kusaga kilo moja, thomu na tangawizi kijiko kimoja cha supu,vitunguu maji vilivyokatwakatwa vipande vidogona kotimiri iliyokatwakatwa vipande vidogo vikombe viwili na chumvi kiasi.
Mahitaji mengine ni pilipili mbichi iliyosagwa,kijiko cha chai kimoja,
Pilipili manga kijiko cha chai kimoja,bizari ya pilau kijiko cha chai kimoja, giligiliani iliyosagwa kijiko cha chai,mdalasini wa unga kijiko cha chai,chenga za mkate kikombe kimoja na mayai mawili.
Vipimo vya wali:
mchele vikombe sita, vitunguu vikubwa kiasi vitano,mafuta ya kupikia kikombe kimoja cha chai, nyanya kubwa zilizokatwakatwa vipande vidogo kwa mtindo mmoja,pilipili mbiga ya kijani na pilipili mbichi nzima.
Mahitaji mengine ni masala kijiko komoja cha supu, hiliki ya unga kijiko cha chai,mtindi wa ‘yoghurt’ nusu kikombe, nyanya ya kopo vijiko vya supu viwili, chumvi kiasi mafuta ya kunyunyizia katika wali vijiko vya supu viwili na rangi za biriani unazotaka.
Jinsi ya kutayarisha:
Wakati wa kupika Kababu, changanya nyama na vitu vyote isipokuwa mayai na chenga za mkate, tia mayai yaliyopiwa pamoja na chenga za mkate na changanya vizuri, yatengeneze katika umbo la mayai na kisha panga katika trei ya oveni.
Baada ya hapo weka katika oveni na uziache kwa muda wa dakika 10 na epua na kuziweka katika bakuri utakalopikia biriani.
Tengeneza masala kwa kutia mafuta katika sufuria na kisha weka vitunguu na kanga hadi viwive na kuwa vya rangi ya hudhurungi, weka nyanya ,pilipili mbichi,pilipili mboga, bizari zote chunvi na kisha kanga kwa kuda mfupi.
Baada ya hapo weka nyanya ya kopo kisha tia mtindi na uache kidogo katika moto, mimina juu ya kababu na uchanganye pamoja, chenmsha mchele na acha uwive na baada ya hapo mimina juu ya masala na weka rangi za biriani unazotaka juu ya wali na kisha nyunyizia mafuta kidogo na changanya mchanganyiko huo.
Funika kwa muda wa dakika 20 na baada ya hapo chakula chako kitakuwa tayari kwa kuliwa .
Tukutane wiki ijayo katika mada nyingine, wasiliana nami kwa barua pepe joymagoti87@yahoo.com au 0715933815.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment